WAFICHUENI WASAMBAZAJI NA WAUZAJI WA MADAWA YA KULEVYA ILI KUOKOA VIJANA - KABEHO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAFICHUENI WASAMBAZAJI NA WAUZAJI WA MADAWA YA KULEVYA ILI KUOKOA VIJANA - KABEHO

Na Mwamvua Mwinyi, ChalinzeWANANCHI wametakiwa kufichua watu wanaojihusisha katika matumizi ya madawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na wasambazaji na wauzaji ili kupunguza tatizo la kuweka rehani baadhi ya vijana ambao ndio nguvu kazi. Akizungumza Chalinze,Bagamoyo mkoani Pwani ,katika mbio za mwenge wa uhuru ,kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ,Charles Kabeho alisema ,matumizi ya madawa hayo ni janga kubwa ndani ya jamii.
"Nawaomba wananchi msiogope kuwafichua wahusika hata kama ni ndugu yako ,jirani, kwani wanaojiingiza katika wimbi hilo wapo miongoni mwetu. Jengeni ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo jeshi la polisi ,ili hali kukabiliana na tatizo hili" alisisitiza Kabeho, akiongeza: "Niwaase ," walioathirika na madawa hayo wajitambue kwa kuacha ,wasikate tamaa,kwani wanaweza kufanya biashara ndogondogo kwa lengo la kujipatia kipato"
Awali mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Alhaj Majid Mwanga akipokea mwenge wa uhuru kutokea Kibaha Mjini alisema, mwenge huo utapitia miradi 15 iliyo... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More