WAFUNGA NDOA WODINI BAADA YA BWANA HARUSI KUSHAMBULIWA NA MAJAMBAZI JANA YAKE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAFUNGA NDOA WODINI BAADA YA BWANA HARUSI KUSHAMBULIWA NA MAJAMBAZI JANA YAKE

 Na Sultani KipingoWapenzi wawili mjini Cape Town, Afrika ya Kusini, wamefunga ndoa hospitalini siku moja baada ya bwana harusi kushambuliwa na majambazi nyumbani kwake .

Muneer Hercules na Maryam Kallie walifunga pingu za maisha katika hospitali ya Melomed Gatesville Jumapili Machi 10, 2019, huku bwana harusi akiwa kitandani na Bi harusi pembeni yake.

Kwa mujibu wa ukurasa wa Facebook wa Melomed Gatesville, Hercules alikimbizwa hospitalini hapo baada ya kujeruhiwa na majambazi nyumbani kwake Jumamosi Machi 9.

"Asubuhi hii Muneer Hercules na Maryam Kallies wamefanya Nikkah mbele ya watu wa familia zao hapa  Melomed Gatesville Hospital. Muneer alishambuliwa usiku wa kuammia leo na kukimbizwa hospitali.” Ameandika  Melomed.

Hata hivyo, shambulizi hilo halikuzuia wapenzi hao kuoana kwa taratibu za Kiislamu hapo hospitali, na mapicha kibao yaliyo kwenye ukurasa wa Melomed yanaweza kukufanya utokwe na chozi.

Maryam alikuwa amevaa shela lake nzuri nyeupe huku mkononi kashikilia maua wakati a... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More