WAGONJWA 20 KUFANYIWA UPASUAJI WA MOYO WA KUFUNGUA KIFUA NA KUWEKEWA VALVU ZAIDI YA MBILI KATIKA KAMBI MAALUM YA MATIBABU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAGONJWA 20 KUFANYIWA UPASUAJI WA MOYO WA KUFUNGUA KIFUA NA KUWEKEWA VALVU ZAIDI YA MBILI KATIKA KAMBI MAALUM YA MATIBABU

Na Salome Majaliwa - JKCI11/9/2018 Wagonjwa 20 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua na kuwekewa  valvu zaidi ya mbili (milango ya moyo) kwenye kambi maalum ya matibabu inayofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Upasuaji huo unafanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya  Misaada (IIRO) ya nchini Saudi  Arabia.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete  Dkt. Bashir Nyangasa wakati akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Dkt. Nyangasa ambaye pia ni daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu alisema upasuaji huo unafanywa kwa wagonjwa ambao valvu zao tatu hazifanyi kazi vizuri hivyo basi zinabadilishwa na kuwekwa valvu  za bandia.
“Kambi hii ni ya siku saba tangu ilipoanza tumefanya  upasuaji na kubadilisha valvu kwa wagonjwa tisa ambao hali zao zinaendelea vizuri na hi... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More