WAGONJWA WA MACHO 300 NCHINI WAFANYIWA UPASUAJI NDANI YA SIKU TANO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAGONJWA WA MACHO 300 NCHINI WAFANYIWA UPASUAJI NDANI YA SIKU TANO

Na WAJMW-DODOMAWatu wenye matatizo ya macho takribani 700 wamefanyiwa uchunguzi na kati ya hao wagonjwa 300 waliobainika kuwa na matatizo ya macho wamefanyiwa upasuaji na kurejeshewa hali ya kuona vizuri.Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja wa Mpango wa Huduma za Macho kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Bernadetha Shilio wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya siku ya afya ya macho duniani kilichofanyika mapema leo katika viwanja vya Nyerere jijini Dodoma.“Siku ya afya ya macho duniani ina lengo kuu la kuhamasisha utekelezaji wa dira ya kimataifa ya kutokomeza upofu unaozuilika ifikapo mwaka 2020, na kutathmini haki ya kuona kwa wote ambapo mwaka 2003 serikali ya Tanzania iliungana na mataifa mengine duniani katika kutekeleza azimio hilo”. Alisema Dkt. ShilioDkt. Shilio amesema Serikali ya Tanzania inashirikiana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku ya afya ya macho ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa jamii, kutoa huduma za uchunguzi wa macho ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More