WAHARIRI MNA NAFASI KUBWA YA KUELIMISHA JAMII ILI KUPUGUZA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WACHANGA-UNICEF - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAHARIRI MNA NAFASI KUBWA YA KUELIMISHA JAMII ILI KUPUGUZA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WACHANGA-UNICEF

Shirika la kuhudumia watoto duniani (UNICEF) Tanzania limesema vifo vya watoto wachanga na mama wajawazito ni miongoni mwa changamoto inayozikumba nchi nyingi duniani, ikiwemo Tanzania. Kufuatia hali hii, shirika hilo limesema wadau, wakiwemo wahariri ,waandishi wa habari na jamii kwa ujumla wana nafasi ya kuelemisha jamii, ili kusaidia mama wajawazito na watoto wachanga kuepuka vifo zisivyo vya lazima wakati na baada ya kujifungua.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika la kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Tanzania, Usiah Mkoma amesema katika semina ya wahariri, iliyoandaliwa na kampuni ya True Vision Production kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na UNICEF katika hoteli ya Regency iliyopo Mikocheni, Dar es Salaam kuwa wahariri kutoka vyombo vya habari nchini wanaweza kutumia nafasi zao na kalamu zao katika kusaidia kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kumsaidia mama mjamzito kwenda kliniki ili avuke salama yeye na mtoto atakayemzaa.
Umbali, ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More