WAHASIBU WATATU WA TTCL KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA WIZI WAKIWA WATUMISHI - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAHASIBU WATATU WA TTCL KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA WIZI WAKIWA WATUMISHI

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Wahasibu watatu wa shirika la Mawasiliano Tanzania, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za wizi wakiwa watumishi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya sh milioni 57.
Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa serikali Mwandamizi, Patrick Mwita, amewataja washtakiwa hao kuwa ni, Mercy Semwenda (49) Flora Bwahawa (54) na Hawa Tabuyanja(54).
Mbele Hakimu Mkazi, Augustine Rwizile imedaiwa, mshtakiwa Semwenda peke yake anadaiwa, kati ya Januari Mosi mwaka 2017 na Septemba 21 mwaka 2017 jijini Dar es Salaam, aliiba vocha za muda wa maongezi za TTCl zenye thamani ya sh 44,393,000/ pamoja na fedha za mauzo ya Vocha zenye thamani ya sh milioni 5,914000/
Imedaiwa kuwa, mshtakiwa alifanya uwizi huo kutokana na kamba alikuwa mfanyakazi wa TTCL kama Mhasibu.
Katika shtaka la pili imedaiwa, siku na mahali hapo, washtakiwa wote, waliisababishia Shirika la Mawasiliano Tanzaniq, (TTCL), hasara ya sh. Milioni 57,773,122.
Hata hivyo, washtaki... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More