WAHITIMU SHAHADA ST. JOSEPH, TANZANIA WASAFIRISHWA ITALIA KWA MASOMO YA URUSHAJI SATELLITE YA KWANZA NCHINI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAHITIMU SHAHADA ST. JOSEPH, TANZANIA WASAFIRISHWA ITALIA KWA MASOMO YA URUSHAJI SATELLITE YA KWANZA NCHINI


Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Wahitimu wawili wa Shahada ya Uhandisi wa Umeme na Mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, Tanzania (Bachelor in Electronics and Communications Engeneering) wamesafiri kuelekea nchini Italia katika Chuo Kikuu cha Parma kuendelea na masomo yao ya Shahada ya Uzamili.
Akizungumza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 3), Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Innocent Ngalinda amesema Wanafunzi hao wanaenda Italia kujifunza namna yakurusha Satellite wakati Tanzania ikijiandaa kufanya hivyo, amesema hivi karibuni Wanafunzi wengine Kumi wataelekea India kujifunza masuala hayo.
Prof. Ngalinda amesema Wahitimu wengine wataenda nchini India kujifunza masomo hayo yaurushaji wa Satellite angani, kutokana na India kuongoza katika kurusha Satellite nyingi duniani.
Pia amesema Wahitimu hao wanaenda masomoni Italia ikiwa ni mpango wa ushirikiano wao na Vyuo vya nje ya nchi katika kuwapeleka Wanafunzi kusoma masuala mbalimbali bila gharama yo... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More