Waitara awakumbusha Wakurugenzi kutekeleza maelekezo ya kununua zana za kufundishia watoto wa madarasa ya awali - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Waitara awakumbusha Wakurugenzi kutekeleza maelekezo ya kununua zana za kufundishia watoto wa madarasa ya awali

Naibu Waziri Tamisemi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Mwita Waitara amewakumbusha Wakurugenzi kutekeleza maelekezo ya kununua zana za kufundishia kwa watoto wa madarasa ya awali ili waweze kujifunza kwa vitendo na kukuza ubongo wao.
Waitara alisema kuwa, zana hizo ni muhimu na kwamba zinamsaidia mtoto kujifunza kwa njia rahisi na salama na kumuongezea uelewa katika elimu ya malezi na makuzi.
Alisema tayari serikali ilishatoa maelekezo kwa wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kununua zana za kufundishi kwa wanafunzi wa madarasa ya awali, kwa sababu zina hizo zinasaidia kupanua uelewa wa watoto katika masuala ya elimu, malezi na makuzi.
"Tayari tumeshatoa maelekezo kwa wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya elimu changamshi kwa madarasa ya awali ili waweze kupata elimu bora ya malezi na makuzi," alisema Waitara.
Anaongeza kuwa Mtoto anapotumia zana za kujifunzia kuanzia darasa... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More