Wajasiriamali Nchini Kuendelea Kunufaika na Urasimishaji wa Biashara - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wajasiriamali Nchini Kuendelea Kunufaika na Urasimishaji wa Biashara

Wajasiriamali Nchini kuendelea kunufaika na Mpango wa Kurasimisha Biashara katika mwaka wa fedha 2018/2019 ikiwa ni moja ya hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuwaniunua wajasiriamali hao. 
Akizungumza wakati wa mafunzo kwa Wajasiriamali wa Halmashuri ya Mji wa Njombe yanayolenga kuwajengea uwezo wajasiriamali ili waweze kurasimisha biashara zao na hivyo kuongeza tija na kuchangia katika ujenzi wa Taifa, Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania ( MKURABITA) Bi. Seraphia Mgembe amesema kuwa lengo ni kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha Biashara zao. 
“Tunashukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Bunge kwa kuiwezesha MKURABITA kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi hasa katika eneo la kuwasaidia wajasiriamali wadogo ili warasimishe Biashara zao;’’ Alisisitiza Mgembe 
Akifafanua amesema kuwa mafunzo yakuwajengea uwezo Wajasiriamali hao yameendeshwa kwa siku 10 ambapo kila kundi lil... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More