WAJAWAZITO CHALINZE WAKEMEWA KUTUMIA DAWA ZA KIENYEJI WAKATI WA KUELEKEA KUJIFUNGUA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAJAWAZITO CHALINZE WAKEMEWA KUTUMIA DAWA ZA KIENYEJI WAKATI WA KUELEKEA KUJIFUNGUA

NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE .
HOSPITAL ya wilaya ya Chalinze ,Msoga mkoani Pwani ,inakabiliana na changamoto za uzazi ambapo baadhi ya akinamama wamekuwa wakitumia dawa za mitishamba ili kujifungua haraka hali inayosababisha wakati wa kujifungua kuwa na uchungu mkali ,mtoto kuchoka na kutokwa damu nyingi. 

Mganga mfawidhi katika hospital hiyo Patricia Kihula ,alisema wapo akinamama wajamzito wanaoshikwa uchungu kisha kunywa mizizi ama dawa za kienyeji jambo ambalo ni hatari kwa mama na mtoto. Alisema kwasasa wanaendelea kutoa elimu katika klinik . 

Patricia alisema ,hali hiyo inasababisha mama akiwa tayari kanywa mizizi mchungu unakuwa mkali kabla ya njia kufunguka na mtoto kuchoka toka akiwa tumboni . “Tunatoa elimu kwa jamii wasiwe na tabia hiyo ,”na sisi tumeanza kupambana na tabia hiyo kwa kuwapa chai kabla ya kujifungua kwani tumegundua wanapewa dawa hizo ndani ya chai “. 

” Tumetoa maagizo chai inapaswa kutolewa kituoni hapa hapa ,na chai ikitoka nyumbani tu... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More