WAJUMBE WA BODI NA MENEJIMENTI YA BOHARI YA DAWA YA TAIFA UGANDA (NMS) WATEMBELEA MSD - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAJUMBE WA BODI NA MENEJIMENTI YA BOHARI YA DAWA YA TAIFA UGANDA (NMS) WATEMBELEA MSD

Na Mwandishi WetuWAJUMBE wa Bodi na Menejimenti ya Bohari ya Dawa ya Taifa,nchini Uganda (NMS) wametembelea Bohari ya Dawa (MSD)  kubadilishana uzoefu na kujifunza namna MSD inavyoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya nchini (NHIF).Pamoja na mambo mengine Meneja Mkuu wa NMS Bwana Moses Kamabare ameipongeza MSD kwa kuboresha utendaji wake ikiwa ni pamoja na huduma zake kwa wateja na kufanya mabadiliko makubwa katika mnyororo wa ugavi.Akizungumza na ugeni huo,Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Dkt. Fatma Mrisho amesema ushirikiano wa taasisi hizi mbili ni muhimu sana,hasa kwenye eneo la kubadilishana uzoefu kiutendaji, kwa nia ya kuboresha huduma.Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu amesema MSD imefanya maboresho makubwa kiutendaji,na ni siri kubwa ya mafanikio katika kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) Dkt. Fatma Mrisho (wa pili kulia), akiwaongoza wajumbe hao kwenda kuangalia Ghala la kuhifadhia dawa na ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More