WAKANDARASI WA UMEME VIJIJINI WATAKIWA KUTOFICHA VIFAA VYA UMETA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAKANDARASI WA UMEME VIJIJINI WATAKIWA KUTOFICHA VIFAA VYA UMETA

WAZIRI wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amewataka wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini kutoficha vifaa vya Umeme Tayari (UMETA) wakati wa usajili wa wananchi wanaohitaji kuunganishwa na huduma hiyo. 
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, aliyasema hayo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tanga ambapo alizindua huduma ya umeme katika kijiji cha Magaoni na Kibiboni vilivyopo wilayani Mkinga na Kijiji cha Tingeni na Kwabota vilivyoko wilayani Muheza. 
“ Ni marufuku kwa mkandarasi kuficha vifaa vya Umeta wakati wa usajili wa wananchi, hakikisheni vifaa hivi vinakuwepo na mwananchi awe huru kuchagua kama anahitaji kuunganishiwa umeme kwa kutumia UMETA au kuingia gharama ya kutandaza nyaya ndani ya nyumba yake,”alisema Dkt Kalemani. 
Alisema kuwa, kila mkandarasi amepewa vifaa vya Umeta 250 kwa kila eneo lake la mradi hivyo wana wajibu wa kuhakikisha kuwa, wananchi wanafahamu uwepo wa vifaa hivyo ili kuwapunguzia gharama za kutandaza nyaya ndani ya nyumba. 
Katika mikutano yake na wa... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More