WAKATI UMEFIKA IBRAHIM AJIB AANZE KUFANYIA KAZI ANAYOAMBIWA NA MAKOCHA WAKE - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAKATI UMEFIKA IBRAHIM AJIB AANZE KUFANYIA KAZI ANAYOAMBIWA NA MAKOCHA WAKE

ANAFANYA vizuri katika klabu yake na kwa sasa ndiye mchezaji tegemeo zaidi Yanga SC.
Namzungumzia Ibrahim Ajib Migomba, kiungo mshambauliaji aliye katika msimu wa pili Yanga SC tangu asajiliwe kutoka kwa mahasimu, Simba SC.
Baada ya kukosekana mara mbili katika vikosi vya timu ya taifa vya kocha mpya, Mnigeria, Emmanuel Amunike safari hii Ajib alitarajiwa sana kupewa nafasi. 
Lakini kwa mara nyingine, jicho la Amunike bado halipendezewa na kiungo huyo anayeweza kucheza pia kama mshambuliaji,  japokuwa Taifa Stars itamkosa Nahodha wake, Mbwana Ally Samatta ambaye atakuwa anatumikia adhabu ya kadi za njano.

Pamoja na hayo, winga huyo wa zamani wa Barcelona na Nigeria, Amunike ameimarisha safu yake ya kiungo kwa kumchukua Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kuziba pengo la kiungo mwenzake wa Azam FC, Frank Domayo ambaye majeruhi pia.
Amemuita pia kiungo Shiza Ramadhani Kichuya katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kwa ajili ya mchezo dhidi ya Lesotho katikati ya mwezi huu kufuzu Fainali za K... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More