WAKAZI WAISHIO KANDO YA MTO NGERENGERE WAHAMA MAKAZI YAO KWA MUDA MANISPAA YA MOROGORO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAKAZI WAISHIO KANDO YA MTO NGERENGERE WAHAMA MAKAZI YAO KWA MUDA MANISPAA YA MOROGORO


Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Yespa Manispaa ya Morogoro wakiwa nje ya nyumba zilizozingirwa na maji.

……………………………..


NA FARIDA SAIDY, MOROGORO


Baadhi ya kaya zilizo kandokando ya Mto Ngerengere Mtaa wa Yespa Manispaa ya Morogoro zimezingirwa na maji na kusababisha wakazi wa mtaa huu kuhama  kwa muda, ambapo imeelezwa hali hiyo imesababishwa na Maji kupoteza mwelekeo baada ya sehemu ya mto kuzibwa katika ujenzi wa Reli ya kisasa.


Wakiongea kwa nyakati tofauti wakazi hao wamesema kuwa hali hiyo imesababishwa na maji kupoteza mwelekeo kufuatia ujenzi wa miundombinu ya reli ya kisasa ambao imesababisha maji kujaa katika makazi ya watu.

Aidha wakazi hao wamesema kuwa  hali hiyo ya maji kuingia kwenye maeneo ya makazi imetajwa kusababisha hasara, ambapo licha ya baadhi ya watu kulazimika kuyahama makazi yao kwa muda, pia baadhi ya huduma zimesimama ikiwemo ibada.


Wakazi hawa walio pembezoni mwa mto Ngerengere wamesema kuwa wengi wao wameishi kwa muda mrefu katika maeneo hayo ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More