Wakili Albert Msando Amlipia JPM Deni la Mil 5 Muhimbili - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wakili Albert Msando Amlipia JPM Deni la Mil 5 Muhimbili

Na Sophia Mtakasimba GPLDeni  la shilingi milioni tano kati ya Shilingi 5,364, 814.2 ambalo Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliahidi kulipa ikiwa ni gharama za matibabu ya marehemu Bi. Sabina Kitwae Loita, leo limelipwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako Bi. Sabina alikuwa akipatiwa matibabu.Fedha hizo ambazo zimechangwa na wananchi zimewasilishwa MNH na wakili Albert Msando kwa niaba ya wananchi haoBi. Laila Kitwae ambaye ni mtoto wa marehemu Sabina Kitwae Loita alitoa ombi la kusaidiwa gharama za matibabu ili aweze kuchukua mwili wa marehemu mama yake Agosti 11 mwaka huu wakati Rais Magufuli alipotembelea Muhimbili kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro.Akizungumza na waandishi wa habari leo alipokuwa akikabidhi fedha hizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru, wakili Msando amesema kuwa amelipa fedha hizo baada ya kuchangisha katika mtandao wa kijamii na amewataka wananchi kulipa gharama za matibabu kwa kuwa MNH ina mahitaji ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More