WAKILI MWESIGWA: WAZEE CHUKUENI HATUA MNAPOONA UONGOZI WA CCM UNAYUMBA KATIKA MAENEO YENU - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAKILI MWESIGWA: WAZEE CHUKUENI HATUA MNAPOONA UONGOZI WA CCM UNAYUMBA KATIKA MAENEO YENU

Na Mwandishi Wetu.
Wazee wameshauriwa kutokaa kimya na badala yake kuchukua hatua madhutubi wanapoona uongozi unayumba katika kusimamia uhai na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika maeneo yao.
Ushauri huo ulitolewa juzi na Mwanasheria wa CCM, Wakili wa Kujitegemea Mwesigwa Zaidi wakati akizungumza kwenye kikao cha Wazee, katika Tawi la CCM la Muloganzira lililopo Kata ya Kwembe Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
Amewasihi Wazee hao kuhakikisha wanakemea tabia inayoanza kuota mizizi ndani ya CCM ya kumtegemea mtu badala ya Chama, tabia ambayo alisema ni hatari sana kwa uhai wa CCM kwa kuwa wengi wanaopenda kusujudiwa ndani ya Chama ni watoa rushwa na mafisadi.
Wakili Mwesigwa mewaomba wazee kuwashawishi watoto wao wenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi mbalimbali ndan ya CCM kujitokeza na wasiwe na hofu kwa sababu uongozi wa juu wa CCM uko imara kuhakikisha hakuna mtoa rushwa wala fisadi yeyote atakayenunua uongozi ndani ya CCM.
Amewataka kuziunga mkono juhudi za Mw... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More