WAKULIMA TUMIENI FURSA YA FAHARI KILIMO KUTOKA BENKI YA CRDB – WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAKULIMA TUMIENI FURSA YA FAHARI KILIMO KUTOKA BENKI YA CRDB – WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu, katika kilele cha Maonyesho ya 27 ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane) 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakulima nchini kuchangamkia fursa zinazotolewa na Benki ya CRDB kupitia akaunti ya “FahariKilimo” ambayo ni maalum kwa ajili ya wakulima. 

Akizungumza wakati wa kilele cha maonyesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane) 2019 nchini iliyofanyika kitaifa mkoani Simiyu, Waziri Mkuu alisema akaunti hiyo ya “FahariKilimo” ambayo imeambatana na fursa nyingine za uwezeshaji ikiwamo mikopo kwa wakulima itasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha mnyororo wa thamani wa kilimo nchini.
"Serikali inaridhishwa sana na jitihada kubwa zinazofanywa na Benki hii ya CRDB katika kuboresha sekta ya kilimo nchini. Ubunifu huu wa huduma na bidhaa mnazozitoa kwa wakulima nchini unaambatana na dhamira ya Serikali ya kuje... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More