WAKULIMA WA MBAAZI NA CHOROKO KUNEEMEKA NA SOKO LA UHAKIKA LA MAZAO HAYO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAKULIMA WA MBAAZI NA CHOROKO KUNEEMEKA NA SOKO LA UHAKIKA LA MAZAO HAYO

Na Mwandishi wetu, KondoaWAKULIMA wa Mbaazi na Choroko hapa nchini wanatarajia kuondokana na adha ya mazao yao kukosa soko baada ya wawekezaji kadhaa kujitokeza kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao hayo katika mikoa ya Arusha, Dodoma, Dar es Salaam na Morogoro.
Kauli hiyo ya matumaini kwa wakulima hao imetolewa wilayani Kondoa mkoani Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omari Mgumba, wakati akitoa salaam kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Jimbo la Kondoa, ambapo Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama hicho kwa kipindi cha miaka 3 ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano.
" Kilimo kinategemewa na zaidi ya asilimia 65 ya watanzania, lakini zao la mbaazi limekuwa na matatizo ya soko ndio maana Serikali imeamua kuchukua hatua kwa kuwahamasisha wawekezaji kujenga viwanda vya kusindika mazao hayo hapa hapa nchini, jambo ambalo limeanza kutekelezwa" ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More