Wakurugenzi wapigwa marufuku kusimamia uchaguzi - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wakurugenzi wapigwa marufuku kusimamia uchaguzi

Mahakama Kuu imefuta sheria iliyokuwa inawapa wakurugenzi wa halmashauri mamlaka ya kuwa wasimamizi wa uchaguzi, uamuzi ambao utalazimisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuteua watu wake badala ya kutegemea wateule hao wa Rais, iwapo hautabadilishwa na Mahakama ya juu.


Mahakama Kuu pia haijaiamuru Serikali kubadilisha vifungu vilivyoonekana vinakwenda kinyume na Katiba baada ya watetezi, wanaharakati wa haki za binadamu na vyama vya siasa kufungua kesi hiyo wakitaka vitamkwe kuwa batili.


Jaji Atuganile Ngala, ambaye alisaidiana na majaji Benhajj Masoud na Firmin Matogolo, alitoa uamuzi huo jana katika kesi hiyo ya kikatiba iliyofunguliwa mwaka 2018


Katika kesi hiyo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mwanachama wa Chadema, Bob Wangwe, aliyekuwa mdai pekee, alikuwa anapinga wakurugenzi hao wa halmashauri za wilaya, manispaa na au majiji kuwa wasimamizi akidai kuwa ni kinyume cha Katiba.


Katika uamuzi wake jana, Mahakama Kuu ilikubaliana na hoja za Wangwe dhidi ya utetezi wa Serikali... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More