WAKURUGENZI WATENDAJI WA HALMASHAURI NCHINI WATAKIWA KUHAKIKISHA FEDHA ZA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI ZINAWAFIKIA WALENGWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAKURUGENZI WATENDAJI WA HALMASHAURI NCHINI WATAKIWA KUHAKIKISHA FEDHA ZA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI ZINAWAFIKIA WALENGWA

Wakurugenzi Watendaji katika halmashauri za wilaya nchini wametakiwa kuhakikisha wanasimamia vema fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini zinawafikia walengwa kama ilivyokusudiwa. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Jason Rweikiza (Mb) wakati wa ziara ya kamati hiyo yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo mkoani Mtwara ikiwa ni pamoja na kujiridhisha namna Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unavyotekelezwa.
Mhe. Rweikiza amekemea tabia ya baadhi ya Wakurugenzi Watendaji katika halmashauri kuelekeza fedha zilizotengwa kwa ajili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika matumizi mengine badala ya kuwanufaisha walengwa ambao ni kaya maskini na kuwataka kuacha tabia hiyo mara moja.“Wakurugenzi Watendaji, mnao wajibu wa kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli za kuboresha maisha ya kaya maskini zote nchini kupitia utekelez... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More