WAKUU WA IDARA ZA ARDHI WATAKAOKALIA HATI ZA ARDHI OFISINI SASA KUKIONA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAKUU WA IDARA ZA ARDHI WATAKAOKALIA HATI ZA ARDHI OFISINI SASA KUKIONA

Na Munir Shemweta, MISENYINaibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amesema kuanzia sasa Mkuu wa Idara ya Ardhi atakayekutwa amekaa na hati ya ardhi kwa muda mrefu   bila kuipeleka ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda kwa ajili ya kukamilisha taratibu za utolewaji hati hiyo basi Mkuu huyo ataondolewa katika nafasi yake.
Dkt Mabula alisema hayo jana tarehe 15 Machi 2019 alipozungumza na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Misenyi mkoani Kagera akiwa katika ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi.
Kauli hiyo ya Dkt Mabula inafuatia kukuta baadhi ya hati katika halmashauri ya wilaya ya Misenyi zikiwa kwenye masijala ya ardhi tangu mwaka 2017 bila kupelekwa ofisi ya Kamishna wa Ardhi Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kukamilishwa ili wahusika wapatiwe hati.
Alisema, baadhi ya halmashauri alizozitembelea wakati wa ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi amebai... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More