Wakuu wa Mashirika ya Umma Wasiotoa Gawio Serikalini Watakiwa Kujitathimi Kama Wanatosha - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wakuu wa Mashirika ya Umma Wasiotoa Gawio Serikalini Watakiwa Kujitathimi Kama Wanatosha


Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amewataka wakuu wa mashirika ya umma yaliyoshindwa kutoa gawiwo kwa Serikali kujitathimini kama wanastahili kuendelea kuyaongoza.
Dk Mpango amesema hayo leo Julai 10, 2018 jijini Dar es Salaam wakati akifungua kongomano la kujadili jukumu la taasisi za umma katika utekelezaji wa sera ya viwanda lililoandaliwa na Taasisi ya Uongozi.
Akisoma hotuba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyemtuma kumwakilisha, Dk Mpango alisema kuna jumla ya mashirika ya umma 270.
"Mimi katika nafasi ya waziri wa fedha na mipango, siridhiki na mashirika ambayo hayatoi gawio kwa Serikali," amesema Dk Mpango
“Wakuu wa mashirika husika na bodi wajitathimimi na nimekwisha muagiza Msajili wa Hazina, achambue na kufuatilia kwa karibu mienendo wa biashara na uongozi wa mashirika yote ili yale yasiyoenda vizuri tuondokane nayo lakini wahusika wawajibishwe,hatutaki kurudia makosa ya zamani," ameongeza
Amesema mashirika 232 yanamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100, mawili asilimia ... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More