Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara Kushiriki katika Mafunzo ya Uongozi - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara Kushiriki katika Mafunzo ya Uongozi

Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa hamsini na mbili wa Tanzania Bara wanatarajiwa kushiriki katika programu ya mafunzo ya uongozi kwa kipindi cha wiki moja kuanzia Jumatatu ya tarehe 3 Disemba, 2018 hadi Ijumaa ya tarehe 7 Disemba, 2018, mkoani Dodoma. 
Warsha hiyo ya mafunzo ambayo imeandaliwa na Taasisi ya UONGOZI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) itafunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) leo. 
Kwa mujibu wa Taasisi ya UONGOZI, programu hii ya mafunzo ya uongozi, ni ya kwanza ya aina yake iliyoandaliwa mahususi kwa ajili ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa. 
“Lengo la programu hii ni kuimarisha uwezo wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala katika kufanya maamuzi ya kimkakati, kuongoza watu na kusimamia rasilimali nyingine, pamoja na kujijengea sifa binafsi za uongozi,” alisema Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof. Joseph Semboja. 
Prof. Semboja pia a... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More