WALIMU KINGS KIZIMBANI KWA KUFANYA KAZI NCHINI BILA KIBALI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WALIMU KINGS KIZIMBANI KWA KUFANYA KAZI NCHINI BILA KIBALI

Na Karama Kenyunko, Michuzi TVWALIMU wanne, raia wa Kenya,  wanaofundisha shule ya msingi na Sekondari ya  Kings na Mtanzania mmoja, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kufanya kazi nchini bila ya kuwa na kibali.
 Akisoma hati mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile, wakili wa serikali Faraji Nguka, amewataja washtakiwa hao kuwa ni.Esrom Maina, (45), Ruth Njuguna (30), Joseph Kuria (30), Charles Sakawa (32) na mtanzania Stella Bizulu (44).
Imedaiwa kati ya Septemba 2018 na Machi 18, 2019 huko katika shule  ya msingi na Sekondari ya Kings iliyoko eneo la Goba ndani ya Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam,  washtakiwa hao raia wa Kenya walikutwa wakifanya kazi ya ualimu katika shule hiyo bila ya kuwa na kibali kutoka idara ya Uhamiaji.
 Katika shtaka la pili  imedaiwa, siku na mahali hapo mshtakiwa Bizulu,  akiwa kama Meneja wa shule hiyo, aliwaajiri walimu hao bila ya kuwa na kibali cha kufanya kazi nchini kutoka Uhamiaji.
Ha... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More