Walimu waliokuwa wanafanya kazi chini ya mti wakabidhiwa ofisi na RC Makonda (Video) - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Walimu waliokuwa wanafanya kazi chini ya mti wakabidhiwa ofisi na RC Makonda (Video)

Kilio cha muda mrefu cha walimu wa shule ya msingi Vijibweni Wilaya ya Kigamboni kufanya kazi chini ya Miti, kwenye vikorido,kwenye madawati na kujisaidia kwa majirani kutokana na ukosefu wa ofisi ya walimu leo kimepatiwa ufumbuzi baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kuwapatia ofisi ya kisasa yenye hadhi ya kimataifa.Ofisi hiyo ya kisasa aliyokabidhi RC Makonda ujenzi wake umegharimu zaidi ya Shilingi Milioni 200 ambapo ndani yake ina ukumbi mikutano, Ofisi ya mwalimu mkuu, Mwalimu mkuu msaidizi,ofisi ya walimu wote, Chumba cha kuhifadhi mitihani, stoo, sehemu ya mapokezi, chumba cha kubadilishia nguo, vyoo vya kisasa na bafu huku ikiwa imefungwa viyoyozi (AC) ili kuhakikisha walimu wanafanya kazi kwa uhuru.


Akizindua ofisi hizo RC Makonda amesema dhamira yake ya kuhakikisha walimu wanafanya kazi katika mazingira bora ipo palepale kwakuwa anatambua thamani ya mwalimu ni kubwa kwenye jamii hivyo wanastahili kupewa heshima.


Aidha RC Makonda ameishukuru Kampuni ya CR... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More