Waliobambikiwa Kesi ya Mauaji na Polisi Waachiwa Huru, DPP Ang’aka - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Waliobambikiwa Kesi ya Mauaji na Polisi Waachiwa Huru, DPP Ang’aka

Mkurugenzi wa Mashtaka, Biswalo Mganga, akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) nakala ya hati ya mashtaka ya mauaji dhidi ya wakazi wawili wa Tabora ambao ilibainika wamebambikiwa na askari wa kituo cha Polisi Tabora baada ya ofisi yake kufanya uchunguzi.

Na ADELINA JOHNBOSCO, Habari MaelezoSerikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeeleza kuchukizwa na kitendo cha Polisi wilaya ya Tabora kuwabambikizia wananchi wawili kesi ya mauaji wakati wakijua ni uongo. Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Mkurugenzi wa Mashataka (DPP), Biswalo Kachele Mganga (pichani), wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO, jijini Dodoma leo.Kitendo cha kubambikiziwa kesi ya mauaji kilibainika baada ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kufanya uchunguzi uliotokana na malalamiko kwenye barua ya wazi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, iliyochapishwa kwenye gazeti la Majira, toleo la tarehe sita ya mwezi Machi 2019. “Baada ya... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More