Waliopoteza maisha ajali ya moto wafikia 57 - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Waliopoteza maisha ajali ya moto wafikia 57

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro Wilbroad Mutafungwa,  amesema leo majira ya saa mbili, asubuhi, gari lililobeba tenki la mafuta lililokuwa likielekea barabara kati ya Iringa na Dodoma, ghafla lilipinduka na mafuta yakaanza kumwagika.


Wananchi walikwenda kuchota mafuta hayo, lakini muda mchache baadaye moto ukaanza kuwaka, na mpaka sasa takribani watu 57 wamepoteza maisha.


Aidha Kamanda Mutafungwa amesema katika tukio hilo, wamekuta pikipiki zaidi ya 10 ambazo zimeteketea kwa moto.


Kamanda huyo amesema kwa sasa wamefanikiwa kuuzima moto huo na taratibu zingine zinafuata ili kubaini idadi kamili ya majeruhi na vifo. Zoezi hili litakwenda sambamba na utambuzi wa majina ya waliopoteza maisha.Tweet


Source: Kwanza TVRead More