WALIOVAMIA SWAGASWAGA WAPEWA SIKU 14 KUONDOKA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WALIOVAMIA SWAGASWAGA WAPEWA SIKU 14 KUONDOKA

Mkuu wa wilaya ya Kondoa Sezaria Makota ametoa siku 14 kwa wananchi wote waliovamia hifadhi  ya pori la akiba la Swagaswaga kuondoka ndani ya hifadhi kabla ya kuondolewa kwa nguvu. Ameyasema hayo alipokuwa akiongea katika mikutano ya hadhara  na wananchi wa mitaa ya Mongoroma na Serya ili iliyofanyika katika maeneo hayo.
Aliongeza kuwa serikali inayafanya hayo ili kuendelea kuhifadhi rasilimali muhimu zilizomo ndani ya hifadhi hiyo ili ziongezeke na kuongeza idadi ya watalii ambao watakuja kwa wingi kupumzika ndani ya hifadhi baada viongozi mbalimbali kuhamia Dodoma. “Ni wakati maalum sasa watu waheshimu mipaka ya hifadhi na wasikae ndani ya hifadhi sababu serikali ina mkakati  wake madhubuti wa kuendeleza hifadhi zote kama sehemu ya kuongeza pato la nchi”.Alisema Makota
Aliongeza kuwa kaya zote zilizomo ndani ya hifadhi na zinafahamika hivyo ni wakati muafaka kwa wao kuondoka  na kuacha kulima kwa mwaka huu kwani wapo waliokata misitu na kuandaa mashamba. “Pia kwasasa serikali... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More