WALIOZEMBEA KUSIMAMIA,KUJENGA MRADI WA MAJI UKALAWA-KITOLE, MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUISAIDIA POLISI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WALIOZEMBEA KUSIMAMIA,KUJENGA MRADI WA MAJI UKALAWA-KITOLE, MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUISAIDIA POLISI

Kutokua makini katika uratibu, usimamizi na ujenzi wa mradi wa maji mkoani Njombe kumewaweka matatani baadhi ya watendaji wa serikali na wakandarasi waliopewa dhamana ya kujenga na kufikisha majisafi na salama kwa wananchi.

Mradi uliotiliwa shaka wa Ukalawa na Kitole umesubiriwa na wananchi kwa zaidi ya miaka mitano na bado umekua butu kukidhi kiu ya wakazi wa vijiji vya Ukalawa na Kitole. Mradi huo umejengwa na kampuni ya Kihanga Farm International iliyolipwa kiasi cha Shilingi Milioni 532 kati ya Shilingi Milioni 562.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameelekeza wahusika walioshiriki katika mradi huo wakiwamo Watalaam wa maji wa Serikali popote walipo, Mhandisi Mshauri wa mradi na Mkandarasi wa mradi wasaidie Jeshi la Polisi kupata undani wa taarifa zinazohusu mradi, ikiwamo malipo yaliyofanyika wakati wananchi hawapati maji.

Mhe. Aweso (Mb) katika kikao kilichodumu kwa saa sita kilichowakutanisha watalaam wa maji, na baadhi ya walioshiriki kati... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More