Waliyoiponda Nguo Yangu Wataiiga Hivi Karibuni- Calisah - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Waliyoiponda Nguo Yangu Wataiiga Hivi Karibuni- Calisah

Model na mwanamitindo maarufu Bongo, Calisah Abdulhamiid amefunguka na kudai kivazi alichovaa siku ya mashindano ya Miss Tanzania 2018 kitaigwa sana na watu hapo baadae.


Calisah alitengeneza headlines Kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana na vazi hilo ambalo lilisemekana kuwa limekaa kwa kama blauzi ya kike kutokana na material yake na rangi.


Baada ya kipindi sana na watu kwa ajili ya kivazi hicho, Calisah amesema haoni tatizo la nguo ile na wanaomponda ndio watakuwa wa kwanza kuiga hapo baadae.


Kwenye mahojiano na Global Publishers, Calisah amesema kuwa sheria namba moja ya mitindo ni kuvaa chochote kile ili mradi kinamfanya mtu awe huru na mashabiki wasikariri kama kuwa mwanamitindo lazima uvae suti.Ile nguo haina vifungo na kitu pekee kinachokufanya ujue nguo kama ni ya kike au ya kiume ni vifungo na zipu vinavyowekwa upande wa kushoto au kulia. “Ilikuwa na kamba kamba za silva na ni ya kiume kabisa. Najua wanaosema hivi utawaona wakiniiga hivi karibuni“. 


The post ... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More