WANA YANGA KUAMUA HATIMA YAO MKUTANONI LEO MBELE YA WAZIRI MWAKYEMBE…MANJI ATAKUWEPO - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WANA YANGA KUAMUA HATIMA YAO MKUTANONI LEO MBELE YA WAZIRI MWAKYEMBE…MANJI ATAKUWEPO

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MKUTANO Mkuu wa mwaka wa klabu ya Yanga SC unatarajiwa kufanyika leo katika Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam huku mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison George Mwakyembe.
Katibu wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online asubuhi ya leo kwamba, pamoja na Waziri Mwakyembe aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu, Yussuf Manji amepelekwa mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo.
“Kadi za uanachama mpya za Posta na za zamani zote zitatumika. Jambo la kuzingatia ni kwamba lazima ziwe hai zimelipiwa ada na mwanachama lazima awepo katika kitabu ch orodha ya wanachama wa klabu na tawi lake,”amesema Mkwasa.
Yanga imekuwa chini ya Kaimu Mwenyekiti, Clement Sanga kufuatia kujiuzulu kwa Yussuf Manji Mei mwaka jana

Ikumbukwe Yanga imekuwa chini ya Kaimu Mwenyekiti, Clement Sanga kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti, Yussuf Manji Mei mwaka jana.
Manji aliingia Yanga mwaka 2006 k... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More