WANACHAMA WA YANGA KWA KAULI MOJA WAKUBALI MABADILIKO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WANACHAMA WA YANGA KWA KAULI MOJA WAKUBALI MABADILIKO

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Wanachama wa Yanga kwa kauli moja wamfikia hatua ya makubaliano kwenda katika mfumo wa mabadiliko ambao utaruhusu timu hiyo kuwa Kampuni.
Yanga iliyofanya mkutano wake leo Jijini Dar Es Salaam, ulianza kwa hotuba ya Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe na kuwaasa wanachama wa Yanga wafanye maamuzi sahihi ili kuweza kuiweka timu yao katika dira nzuri.
Dkt Mwakyembe amesema kuwa Yanga ni alama ya ukumbusho barani Afrika kama klabu iliyoweza kusaidia upatikanaji wa uhuru wa Tanganyika na bara la Afrika.
"Yanga imechaguliwa kuwa alama ya ukumbusho barani Afrika kama moja ya vilabu vilivyobeba alama ya uhuru wa Tanganyika na uhuru wa bara la Afrika, Yanga ni klabu kubwa na yenye historia yake ndania ya nchi hii , "amesema Dkt Mwakyembe.
Dkt Mwakyembe amesema uwekezaji katika klabu za mpira ni jambo lisilokwepeka na hata serikali inaunga mkono suala hilo kulingana na mahitaji yanayohitajika ili kuwa na soka la ushindani.Pia amesema... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More