WANAFUNZI MANYARA NA SINGIDA WANUFAIKA NA SWASH - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WANAFUNZI MANYARA NA SINGIDA WANUFAIKA NA SWASH

WANAFUNZI wa vilabu 1,700 vya afya na usafi mashuleni kwenye wilaya za Mbulu, Hanang Mkoani Manyara na Mkalama Mkoani Singida, wamenufaika na elimu ya afya waliyopatiwa kupitia kituo cha pembe nne za utamaduni Haydom (4CCP). 
Ofisa miradi wa kituo cha pembe nne za utamaduni Haydom (4CCP) Nelson Faustine aliyasema hayo wakati wa kongamano la wanachama wa klabu za afya na usafi mashuleni lililohusisha walimu na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari. 
Faustine alisema wametoa mafunzo ya matumizi sahihi ya vyoo, vibuyu chirizi, kichanja, shimo la taka, usafi binafsi na namna ya kutibu maji. "Tumepanga kuongeza vifaa vya usafi, kuandaa majarida yanayohusiana na afya na kuhamasisha matumizi ya muongozo wa kitaifa wa maji, elimu ya afya na usafi wa mazingira mashuleni," alisema. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Horace Kolimba alisema aliagiza shule zote za halmashauri hiyo kuanzisha klabu za afya na usafi mashuleni. Kolimba alisema wametoa maagizo kwa watendaji ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More