WANAFUNZI WA CHUO KIKUU MZUMBE WAASWA KUJINOA NA MTOHANI YA BODI YA NBAA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU MZUMBE WAASWA KUJINOA NA MTOHANI YA BODI YA NBAA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu Mzumbe Tawi la Dar es Salaam katika kozi ya uhasibu wameaswa kujinoa vizuri katika mitihani ya Bodi ya Uhasibu Nchini (NBAA) ili waweze kufanya vizuri katika mitihani hiyo ambayo itaanza hivi karibuni.
Akizungumza na wanafunzi wa wa Chuo Kikuu Mzumbe Tawi la Dar es Salaam Afisa Mitihani wa Bodi ya Uhasibu (NBAA) Humphre Sympholian amesema kuwa mitihani ya bodi sio migumu kinachotakiwa kwa wanafunzi kujiandaa vizuri ambapo wanaweza kufanya vizuri.
Amesema kuwa kwa wale wanaofanya kazi katika kipindi kilichobaki waweze kuomba ruhusa ya kwa ajili ya kujiandaa na mitihani hiyo na kuweza kupata cheti mahususi kwa ajili ya uhasibu (CPA).Sympholian amesema kuwa mitihani hiyo wamekuwa mtihani wa bodi hiyo hauna upendeleo hivyo kila mtu atapata alichokipanda katika kujiandaa kwake na huo mtihani.
“Hatuna upendeleo kwani wanaosimamia sio ndio wanaosahihisha na kusahihisha huko hakuna majina ya wanafunzi kilichopo ni namba tu ambapo h... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More