WANAFUNZI WATANO WAIBUKA KIDEDEA SHINDANO LA ANDIKA CHALLENGE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WANAFUNZI WATANO WAIBUKA KIDEDEA SHINDANO LA ANDIKA CHALLENGE


Taasisi ya Dr Ntubayaliwe imepongezwa kwa Kubuni shindano la kutunga hadithi kwa wanafunzi wa shule za msingi, kitendo kinachosaidia kuibua na kukuza vipaji vya wanafunzi nchini.
Kaimu Afisa elimu wa Manispaa ya Kinondoni Mwalimu Martha  Kusaga ametoa pongezi hizo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kutangaza na kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la Andika Challenge la kutunga hadithi zenye maana kwa wanafunzi wa shule za msingi za manispaa za Kinondoni na Ubungo.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Dr Ntuyabaliwe Foundation Bi. Jacquiline Mengi amesema baada ya kuendesha shindano hilo kwa manispaa mbili za Dar es salaam kwa mafanikio makubwa, sasa shindano hilo litawashirikisha  wanafunzi wa shule za msingi za Tanzania nzima.
Amesema shindano hilo litadumu kwa miezi mitatu na washiriki wanatakiwa watume hadithi  kupitia sanduku la barua 163, Dar es salaam, huku kila mshiriki aandike jina lake, jina la shule yake, wilaya na mkoa atokao, na mwisho wa kuwasilisha hadithi ni mwezi Novemba mwaka huu. Hadithi zitakazoshinda zitachapishwa kwenye vitabu na kusambazwa katika maktaba mbalimbali za shule.
 Jumla ya hadithi 1,202 kutoka wanafunzi wa shule za msingi 137 za manispaa za Kinondoni na Ubungo zilipokelewa na kushindanishwa, ambapo  Mshindi wa kwanza alikuwa  Nurath Komba kutoka shule ya msingi Tandale Magharibi.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na Agnes Charles wa shule ya msingi Uzuri, huku Arsernia Charles akishika nafasi ya tatu, na Zulfa Miraji wa shule ya msingi Mtangani, na Aisha Hialai wa shule ya msingi Londa wakishika nafasi za nne na ya tano. Washindi wote na shule wanazotoka walikabidhiwa zawadi mbalimbali, zikiwemo kununuliwa sare za shule na vitabu kwa mwaka mzima, kufunguliwa akaunti ya benki.Kaimu Afisa elimu wa Manispaa ya Kinondoni Mwalimu Martha  Kusaga akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi wa washindi wa shindano la kutunga hadithi kwa wanafunzi wa shule za msingi lililohisisha wilaya mbili za jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mtendaji wa Dr Ntuyabaliwe Foundation Bi. Jacquiline Mengi akitoa historia ya taasisi ya Dr Ntuyabaliwe pamoja na shindano la shindano la kutunga hadithi kwa wanafunzi wa shule za msingi lililohisisha wilaya mbili za jijini Dar es Salaam.Kaimu Afisa elimu wa Manispaa ya Kinondoni Mwalimu Martha  Kusaga (kushoto) akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza kwenye shindano la kutunga hadithi kwa wanafunzi wa shule za msingi, Nurath Komba kutoka shule ya msingi Tandale Magharibi. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Dr Ntuyabaliwe Foundation Bi. Jacquiline Mengi. Baadhi ya wanafunzi walioingia kwenye tano bora ya shindano la kutunga hadithi kwa wanafunzi wa shule za msingi wakipokea zawadi zao zilizodhamniwa na taasisi ya Dr Ntuyabaliwe lilihusisha wilaya ya Kinondoni na Ubungo.Meza kuu ingiongozwa na Kaimu Afisa elimu wa Manispaa ya Kinondoni Mwalimu Martha  Kusaga akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi watano walioibuka kidedea kwenye shindano la kutunga hadithi kwa wanafunzi wa shule za msingi lililoshirikisha shule mbalimbali zilizopo kwenye wilaya mbili za jijini Dar es Salaam.Walimu wa shule zilizotoa washindi watano wa shindano la kutunga hadithi kwa wanafunzi wa shule za msingi wakiwa kwenye picha ya pamoja na meza kuumara baada ya kukabidhiwa zawadi zao.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Source: Issa MichuziRead More