Wanaharakati hawa watatu watunukiwa tuzo mbadala ya Nobel wakiwa Jela - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wanaharakati hawa watatu watunukiwa tuzo mbadala ya Nobel wakiwa Jela

Wanaharakati watatu wa haki za binadamu kutoka Saudia walioko jela watunukiwa tuzo mbadala ya Nobel na taasisi ya Nobel mjini Stolkholm.Pia wapinga rushwa kutoka Guatemala watunukiwa tuzo ya heshima. Washindi wa tuzo maalum ya haki za binadamu au tuzo mbadala ya Nobel wametangazwa leo hii mjini Stolkholm Sweden. Tuzo hiyo imetunukiwa watetezi watatu wa haki za binadamu wakisaudi waliofungwa jela pamoja na wanaharakati wa kupinga rushwa kutoka Amerika Kusini.Taasisi ya tuzo hiyo mjini Stolkholm imesema dolla 113,400 zinazoambatana na tuzo hiyo mbadala ya Nobel zitagawanywa kwa washindi Abdullah al Hamid,Mohammad al-Qahtani na Waleed Abu al Khair wote wa Saudi Arabia kutokana na juhudi zao za kijasiri zinazosimamia misingi ya haki za binadamu ya kimataifa,ili kuleta mageuzi katika mfumo wa kidhalimu wa kisiasa nchini Saudi Arabia.


Tuzo  ya heshima ya mwaka huu imetunukiwa Thelma Aldana wa Guatemala na mkolombia Ivan Velasquez kutokana na mchango wao mkubwa katika kuyafichua matumizi... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More