Wanajeshi 7 wa Umoja wa Mataifa kutoka mataifa haya wauawa nchini DR Congo - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wanajeshi 7 wa Umoja wa Mataifa kutoka mataifa haya wauawa nchini DR Congo

Umoja wa Mataifa umesema walinda wake amani wapatao 7 wameuawa katika mapigano yaliyozuka karibu na mji wa Beni kaskazini mwa Kivu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Ni eneo lililoathiriwa zaidi na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini humo. Bado haijajulikana ni kundi gani la waasi limehusika na mashambulizi.Kwa mujibu wa BBC, Akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya tukio hilo, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema wanajeshi hao waliokufa, 6 ni kutoka Malawi na 1 Tanzania.


”..Walinda amani wameuawa wakati wa operesheni ya pamoja iliyokuwa ikifanywa na Kikosi cha Kulinda amani cha Umoja wa Mataifa na Jeshi la Congo dhidi ya kundi LA Allied Democratic Foirces linalojulikana kama ADF.


”Taarifa za awali zinaonesha kuwa walinda amani wengine 10 wamejeruhiwa na mmoja hajulikani alipo”. Amesema Dujarric


Walinda amani kadhaa wa jeshi la Congo pia wameripotiwa kuuawa ama kujeruhiwa katika operesheni hiyo.


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ametuma salamu za ram... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More