Wananachi wa Mikoa ya Nyanda za juu kusini watakiwa kushiriki maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wananachi wa Mikoa ya Nyanda za juu kusini watakiwa kushiriki maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji

Na Mwandishi wetu, Dar es SalaamBARAZA la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limewataka wananchi wa Mikoa Nyanda za Juu Kusini kushiriki maonyesho ya bidhaa za wajasiriamali na huduma za mitaji yatakayo fanyika katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe mjini Mbeya kuanzia tarehe 19 hadi 23, Octoba, 2018 ili kujionea fursa za uwezeshaji kuelekea katika uchumi wa viwanda.
Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Bi. Beng’i Issa alisema hayo jana jijini Dar es Salaam kuwa maonyesho hayo hayo ni ya bidhaa za wajasiriamali na huduma za mitaji na yatafunguliwa na Waziri Kassim Majaliwa Octoba 20, 2018 na ambayo yanalenga kunadi fursa za uwezeshaji.
“Maonyesho haya yatawezesha upanuaji wa wigo wa masoko ya wajasiriamali wanaotengeneza bidhaa za mikono kwa kutumia mali ghafi za Tanzania,” na hiyo inatoa hamasa kwa wananchi kujikita katika viwanda vidovidogo.
Baraza limeshirikiana na Mifuko ya Uwezeshaji, Vikundi vya kifedha na program za serikali za uwezeshaji kuandaa maonyesho hayo na yatafungwa n... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More