Wananchi kata ya Kala wamlilia RC baada ya kukosa mawasiliano ya simu na radio - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wananchi kata ya Kala wamlilia RC baada ya kukosa mawasiliano ya simu na radio

Wananchi wa kata ya Kala yenye vijiji vitano iliyopo katika wilaya ya Nkasi wamefikisha kilio chao cha kukosa mawasiliano ya simu kwa mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo ili aweze kuwasaidia kutatua kero hiyo ambayo inakwamisha maendeleo ya kata
Kilio hicho kimetolewa wakati wa kusoma risala ya maendeleo ya kata na msoma risala Felix kapoze alipokuwa akielezea changamoto mbalimbali zinazoikabili kata hiyo kwa muda mrefu jambo linalokwamisha utendaji kazi pamoja na kufanya mawasiliano kuwa magumu.
“Changamoto nyingine kubwa ilipo hapa Kijijini kutokuwapo kwa mtandao wa simu, hii inapelekeana kukwama kwa taarifa nyingi hasa katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo hivyo tunaiomba ofisi ya Mkuu wa Mkoa itusaidie kupatikana kwa mtandao wa simu ili kurahisisha mawasiliano,” Alifafanua.
Halikadhalika jambo hilo liliungwa mkono na mbunge wa jimbo la Nkasi Kusini Desderius Mipata wakati akielezea changamoto hiyo na hatua alizochukua kuhakikisha kuwa mawasiliano hayo yanapatinaka na hatim... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More