WANANCHI KISIWANI UNGUJA WAISHUKURU SERIKALI KUPITIA TASAF. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WANANCHI KISIWANI UNGUJA WAISHUKURU SERIKALI KUPITIA TASAF.

Na Estom Sanga-Zanzibar
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- Ksiwani Unguja Bw. Ayoub Mohamed Mahmoud amepongeza jitihada zinazofanywa na Mfuko huo katika kutekeleza maelekezo ya serikali ya kusaidia jitihada za kuwandolea kero ya umaskini wananchi. 
Bwana Mahmoud ambaye pia ndiye Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi amesema TASAF imekuwa kielelezo sahihi na cha kujivunia katika kutekeleza wa sera za kupambana na umaskini kwa kushajihisha wananchi kujiletea maendeleo kwa kutumia nguvu na raslimali zilizoko kwenye maeneo yao. 
Kiongozi huyo ameyasema hayo wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kianga unatekelezwa na Wananchi kwa kushirikiana na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF kupitia utaratibu wa Mfuko huo wa kuendeleza miundombinu ya Afya,Elimu na Maji kwenye maeneo ya Walengwa. 
Mkuu huyo wa Mkoa wa Mjini Magharibi amesema miradi iliyoibuliwa na Wananchi kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na TASAF imeleta mage... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More