WANANCHI WA JIMBO LA LIWALE WAJITOKEZA KWA WINGI KUTIMIZA HAKI YAO YA KIMSINGI YA KUPIGA KURA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WANANCHI WA JIMBO LA LIWALE WAJITOKEZA KWA WINGI KUTIMIZA HAKI YAO YA KIMSINGI YA KUPIGA KURA

Na. Vero Ignatus , Liwale-Lindi
Wananchi wa Liwale na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi asubuhi ya leo katika vituo vya kupigia kura kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge 2018 mkoa wa Lindi.
Kwa mujibu wa Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Liwale Luiza Mlelwa amesema jumla ya wapiga kura waliojiandikisha 55777 na vituo vya kupigia kura 158 wote hawa watapiga kura kumchagua mbunge wao pamoja na diwani kata ya Kibutuka
Balozi Ramadhani Mapuri mjumbe wa Tume ya Taifa ya uchaguzi amesema kuwa ameshuhudia ufunguzi wa vituo, ambapo wapiga kura wamejitokeza kwa wingi na zoezi limeanza kwa wakati hivyo wananchi wasisite kwenda kupiga kura kwani uchaguzi unaendeshwa kwa Amani na Utulivu
Amesema katika vituo vya kupigia kura vya Likongowele Galani pamoja na Kituo cha Ujenzi hali ya uchaguzi ni shwari na wananchi wameendelea kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
Wananchi hao wanapiga kura kuwachagua viongozi wanaowapenda kutoka vyama mbalimbali vya siasa, Abduli Kombo Ngakolwa kutoka chama cha wakulima AAF... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More