WANANCHI WA KIGOMBE WATAKIWA KUACHANA NA BIASHARA ZA MAGENDO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WANANCHI WA KIGOMBE WATAKIWA KUACHANA NA BIASHARA ZA MAGENDO

WANANCHI wa Kijiji cha Kigombe Kata ya Kigombe wilayani Muheza mkoani Tanga wametakiwa kuacha kushiriki kwenye biashara za magendo badala yake watumie maeneo yaliyorasmi kwa kisheria kwa ajili ya upitishaji wa bidhaa. 
Wito huo ulitolewa leo na Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo wakati akizungumza na wananchi hao kwenye mkutano uliofanyika kwenye eneo la sokoni akiwa ameambatana na maafisa wa TRA mkoa wa Tanga. 
Alisema kitendo cha wananchi kuacha kutumia bandari ya Pangani ambayo ipo kusheria wanafanya makosa makubwa na kuwataka kuitumia kupitisha bidhaa badala ya kutumia zile ambazo hazitambuliki ambazo watakapokamatwa watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria. 
“Tumefika hapa kigombe kutoa elimu kwa kuzungumza na wananchi kutokana na changamoto za mara kwa mara biashara za magendo ambazo zimekuwa zikipitishwa eneo hilo na kuona kutumia muda huo kuzungumza na wananchi kuwaambia madhara yake ni yapi”Alisema. ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More