WANANCHI WA KIJIJI CHA NDUNYUNGU WILAYANI LIWALE WASIMAMISHA MSAFARA WA AWESO; WATAKA MRADI UKAMILIKE HARAKA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WANANCHI WA KIJIJI CHA NDUNYUNGU WILAYANI LIWALE WASIMAMISHA MSAFARA WA AWESO; WATAKA MRADI UKAMILIKE HARAKA

Wananchi wa kijiji cha Ndunyungu kilichopo Wilayani Liwale Mkoani Lindi wamelazimika kusimamisha msafara wa Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso alipokuwa njiani kwenda kukagua mradi wa maji wa Barikiwa Wilayani humo. 
Wakiwa na mabango yaliyobeba ujumbe wa kumtaka Nambu Waziri awasaidie kupata maji, pia walieleza adha inayowakumba ya kusubiria maji kwa muda mrefu katika eneo wanalochetea maji jambo ambalo linawasababishia kuchelewa kufanya shughuli za kimaendeleo. 
Baada ya kuwasikiliza kero zao Mheshimiwa Aweso alilazimika kwenda kuona chanzo pekee ambacho wananchi hao wanapata huduma ya maji, ambapo alijionea kisima kinachotumia pampu ya kusukuma kwa mkono na kuongea na wananchi walijitokeza kwa wingi. 
Naibu Waziri Aweso alisema kuwa tayari mkandari anayejenga mradi kwa ajili ya kijiji hicho ameshalipwa pesa kiasi cha shilingi milioni mia moja na moja, hivyo hana sababu za kutokukamilisha mradi na kutokulipa vibarua waliochimba mitaro ya kufukia mabomba ya maji. 
Aidha, akiwa katika ki... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More