WANANCHI WAASWA KUITUMIA OFISI YA URATIBU WA SHUGHULI ZA SMZ - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WANANCHI WAASWA KUITUMIA OFISI YA URATIBU WA SHUGHULI ZA SMZ

Wakati umefika kwa Watanzania wote kuitumia Ofisi ya Uratibu wa shughuli za SMZ Dar es salaam ili kupata maelekezo na Ushauri utakaowawezesha kupata huduma mbali mbali zinazotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ngazi na Sekta zote.
Uamuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa kuanzisha Ofisi hiyo muhimu Mwaka 2013 kuratibu wa Shughuli za Serikali umelenga kuwaondoshea usumbufu Wananchi wanaoishi upande wa Tanzania Bara pamoja na Taasisi za Kimataifa zinazohitaji huduma za Serikali.
Mratibu Mkuu wa Ofisi ya Uratibu wa shughuli za SMZ Dar es salaam Ndugu Issa Mlingoti Ali alitoa kauli hiyo katika Kipindi Maalum cha matayarisho ya maandalizi ya sherehe za kutimia Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 hapo Ofisini kwake Mjini Dar es salaam.
Ndugu Mlingoti alisema huduma za Ofisi hiyo kwa kiasi kikubwa hivi sasa zinatumiwa zaidi na Viongozi Wakuu na wale Waandamizi jambo ambalo bado halijakidhi azma ya kuanzishwa kwake licha ya kwamba yapo mambo mengi na ya msingi yan... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More