WANANCHI WAFUNGUKA KUHUSU ELIMU BORA AU BORA ELIMU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WANANCHI WAFUNGUKA KUHUSU ELIMU BORA AU BORA ELIMU

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
SHIRIKA lisilo la kiserikali la Twaweza limetoa matokeo katika utafiti wao wa Elimu Bora au Bora elimu ambapo wananchi wamefunguka na kudai viwango vya elimu viboreshwe hata kama itawalazimu kulipa ada.
Aidha imeelezwa katika kuchagua shule za Sekondari (kidato cha kwanza)  asilimia 72 ya wazazi huangalia viwango vya ufaulu katika shule, asilimia 6 umbali wa shule na asilimia 18 huangalia umbali wa shule. 
Pia kuhusu wazazi kisaidia uongozi wa shule asilimia 52 ya wazazi hushiriki kwa kuwaadhibu watoto wao, asilimia 22 hushiriki katika harambee za kuchangia shule, asilimia 14 kufuatilia mahudhurio na asilimia 4 kutoa maoni kwenye ukaguzi wa mahesabu ya shule.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi mtendaji wa Twaweza Aidan Eyakuze amesema idadi ya wanafunzi waliojiandikisha darasa la kwanza limeongezeka mara baada ya sera ya elimu bure kuanzishwa ambapo mwaka 2015.
Ambapo watoto walioandikishwa ni milioni 1.5 na mara baada ya sera kuanzishwa watoto milioni 2.2  na 21 waliandikishwa na hiyo inapelekea asilimia 90 ya elimu ya msingi na sekondari hutolewa na Serikali.
Imeelezwa kuwa mitazamo ya wananchi kuhusu elimu bure imebadilika kwa kiasi kikubwa ndani ya miaka 12 ambapo mwaka 2005 asilimia 56 wamesema elimu itolewe bure kwa watoto wao hata kama ni ya kiwango cha chini na kwa mwaka 2017 wananchi 9 kati ya 10 ambao ni asilimia 87 wameeleza ni bora kuongeza viwango vya elimu.
Ameongeza na hata kama itawalazimu kulipia ada  na wangependa Serikali itumie fedha kwenye mpango wa kutoa mafunzo na kuwasaidia walimu kuliko kugawa sare za shule bure ikilenga kuwaondolea wazazi mzigo wa kununua sare hizo.
Imeelezwa kuwa utafiti huo ulifanyika ili kujua elimu waitakayo watanzania ambapo mwaka jana Septemba na Oktoba takwimu zilikusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,786 Tanzania bara bila kuhusisha Zanzibar.
Aidha mdau kutoka Haki elimu  Boniventure Godfrey amepongeza tafiti huo na kueleza wananchi wameona tatizo baada ya kutoa maoni yao kuwa wanataka elimu bora kwa watoto wao hata kama ni ya kulipia na hiyo imedhihirika katika utafiti huo kwa kuonesha mchango wa wazazi katika kuchangia suala la elimu hasa katika suala la miundombinu.
Kwa upande wa  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Othiniel Mnkande ameeleza kwa kuangalia ongezeko la watoto shuleni lazima suala la ubora wa elimu hasa kwa walimu katika kuwawekea mazingira bora katika mafunzo na maslahi pia na kuangalia ubora wa walimu wanaopelekwa mashuleni na ili kwenda kwenye ubora lazima mambo muhimu yaangaliwe kama bajeti na mafunzo bora kwa kuangalia katika hali endelevu.
Wakati huo huo Mwanasiasa na Mwanaharakati Noerakindo Kessy amesema tatizo lililopo ni kutotambua mfumo wa elimu unahitaji nini kwa wakati huu kwani wazazi wengi wanaona ubora katika elimu kwakuwa wanaona changamoto  ambazo walipitia na zilizopo kama kukosa ajira na mmomonyoko wa maadili.
Kessy emeeleza suala la elimu ni la kushirikiana baina ya serikali na wananchi katika kuwalinda walezi wa taifa (walimu) bila kufuata mifumo ya nje.


Source: Issa MichuziRead More