WANANCHI WAJITOLEA KUWEKA ALAMA ZA BARABARANI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WANANCHI WAJITOLEA KUWEKA ALAMA ZA BARABARANI

Na Ahmed Mahmoud,Arusha.
Wananchi wa kata ya Lemara eneo la Nanenane jijini Arusha wameamua kujitolea kwa hali na mali kuweka alama za vivuko viwili vya waenda kwa miguu katika barabara inayoingia katikati ya jiji kwenye eneo linalodaiwa kutokea ajali za mara kwa mara na kusababisha watu wasiyo na hatia kupoteza maisha .
Wanahabari walifika kwenye eneo la nanenane na kushuhudia wakazi wa eneo hilo wakichangishana fedha kwa ajili na kuweka alama hizo huku mafundi wakiendelea na kazi ya kuweka alama hizo ambazo zinatajwa kua ni suluhisho la kuzuia ajali kutokea katika eneo hilo.
Wakazi wa kata hiyo wakizungumzia hatua waliochukua ya kujitolea kwa michango yao wakishirikiana na diwani wao nibaada ya eneo hilo kukidhiri ajali za mara kwa mara ambazo wakati mwingine zinaepukika.
Alfredy Maulid na Pascal Silvery ni wakazi wa kata ya lemara walisema upatikanaji wa kivuko hicho ni mkombozi mkubwa hasa watoto wa shule kuvuka kwa amani kwakua kipindi cha nyuma hali ilikua mbaya ya ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More