WANANCHI WALINDE VYANZO VYA MAJI - PROFESA MBARAWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WANANCHI WALINDE VYANZO VYA MAJI - PROFESA MBARAWA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Profesa Makame Mbarawa amewataka wananchi wanaoishi pembezoni mwa vyanzo vya maji kuvilinda ili viwafaidishe.
Mbarawa ameyasema hayo baada ya kutembelea mradi wa maji wa Mtoni unaozalisha maji Lita Milioni tisa kwa siku.
Akizungumza baada ya kumaliza kukagua chanzo cha Maji cha Mto Kizinga, Profesa Mbarawa amesema kuwa wananchi wanatakiwa kulinda vyanzo vya maji ili kuweza kupafa maji ya uhakika.
Mbarawa amesema mradi wa maji wa mtoni una uwezo wa kutoa maji Lita Milioni tisa kwa siku ambayo inachagiza katika uzalishaji wa maji  katika Mkoa wa Dar es Salaam
Amesema, kwa pamoja wananchi wanatakiwa washirikiane kulinda mazingira kwani Maji ni uhai na watakapoharibu vyanzo  watasababisha ukosefu wa maji ya kutosha.
"Kwa pamoja inabidi tushirikiane na wananchi kuwapa elimu ya umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji, watakapoviharibu vyanzo hivi watasababisha maji kupungua na muda mwingine kuharibu kabisa vyanzo," amesema Profeaa.
Mbali... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More