WANANCHI WANASHUHUDIA MAAJABU MAKUBWA NDANI YA MIAKA MITATU YA RAIS DKT.JOHN MAGUFULI-WAZIRI JAFO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WANANCHI WANASHUHUDIA MAAJABU MAKUBWA NDANI YA MIAKA MITATU YA RAIS DKT.JOHN MAGUFULI-WAZIRI JAFO

Na Said Mwishehe, Dodoma
WAKATI Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais Rais Dk.John Magufuli ikiwa imetimiza miaka mitatu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Suleiman Jafo amesema kuna mambo makubwa ya kujivunia ambayo yamefanyika ndani ya muda huo.
Pia ameeleza hatua kwa hatua namna ambavyo Wizara yake imeshiriki kikamilifu katika kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora katika sekta mbalimbali nchini huku akieleza namna anavyomsukuru Rais Dk.Magufuli kwa namna ambavyo amemuamini na kumteua kuhudumu nafasi hiyo.
Waziri Jafo ambaye ni miongoni mwa mawaziri vijana waliopata nafasi ya kuaminiwa na Rais Magufuli amesema hayo katika mahojiano maalumu na timu ya waandishi wa habari wa Michuzi Blog na Michuzi TV walipofika ofisini kwake katika Jiji la Dodoma.
Ambapo pamoja na mambo mengine mahojiano yalijikita katika kuzungumzia miaka mitatu ya Rais Magufuli na mchango wa Tamisemi katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo kwa Watanza... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More