WANANCHI WATAKIWA KULINDA NA KUVITUNZA VYANZO VYA MAJI ILI VIDUMU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WANANCHI WATAKIWA KULINDA NA KUVITUNZA VYANZO VYA MAJI ILI VIDUMU

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MKURUGENZI wa Kitengo cha Mazingira Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Modester Mushi amewataka wananchi kuendelea kutunza mazingira ili kulinda vyanzo vya maji.
Hayo ameyasema wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji yaliyofikia tamati leo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Mhandisi Modester amesema mazingira yanatakiwa yalindwe katika nyanja zote kuanzia kwenye vyanzo vya maji, miradi inayojengwa na kupata ushauri kutoka Baraza la Mazingira NEMC na Wizara husika.
Amesema, katika sheria ya mazingira ya 2004 imeweka wazi kuwa kwenye kila mradi uandaliwe tathimini itakayoangalia athari za kijamii na kibinadamu. “Mkandarasi anatakiwa afahamu mazingira anayoenda kufanyia kazi, wafanyakazi kuwa na vifaa vya kufanyia kazi, alama elekezi zitakazomuonyesha mwananchi kazi inayofanyika kwa muda huo,”amesema Modester.
Ameeleza, miradi inapomalizik basi hali ya mazingira inatakiwa irudishwe kama awali au kuboreshwa zaidi ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More