WANANCHI WILAYANI BARIADI WARIDHIA KUACHIA MAENEO YAO KUPISHA UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA SIMIYU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WANANCHI WILAYANI BARIADI WARIDHIA KUACHIA MAENEO YAO KUPISHA UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA SIMIYU

Na Stella Kalinga, Simiyu 
Wananchi wa Vijiji vya Igegu na Nga’arita Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi wameridhia kuachia maeneo yao kupisha Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Mkoani Simiyu ambacho kinatarajiwa kujengwa katika eneo la Igegu wilayani .

Wananchi hao wameyasema hayo Septemba 14, 2018 wakati wa uzinduzi wa zoezi la Uthamini na upimaji wa maeneo hayo, ambalo linatarajiwa kumalizika baada ya mwezi mmoja na wiki mbili kuanzia sasa.

Wamesema kuwa wamefurahishwa na hatua ya Serikali kujenga Kiwanja cha Ndege wilayani Bariadi na kwa kuwa ujenzi huo ni suala la maendeleo hawawezi kupinga, huku wakiiomba Serikali kuhakikisha wanalipa fedha za fidia kwa wakati mara tu baada ya kukamilisha zoezi la uthamini na upimaji wa maeneo hayo.

“Kwa kuwa ujenzi wa kiwanja cha ndege ni maendeleo hatuwezi kukataa kutoa maeneo yetu, tumekubali kutoa maeneo ila ombi letu kwa Serikali tunaomba tulipwe fidia ya maeneo yetu kwa wakati na tulipwe kwa haki” alisema Ndaturu M... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More